Ajira Leo

Nafasi ya Kazi UTUMISHI (Mkurabita)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb . Na EA.7/96/01/ J/32 16 Mei , 2019 TANGAZO LA NAFASI YA KAZI (LINARUDIWA) Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa wa kujaza nafasi moja (1) ya kazi kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili .

1.0 MPANGO WA KURASIMISHA RASILIMALI NA BIASHARA ZA WANYONGE TANZANIA (MKURABITA) Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA” ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuwezesha jamii kiuchumi . MKURABITA imeanzishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 2004 kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi unaozingatia utawala wa Sheria . Mpango huu unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais , Ikulu . MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizorasimishwa katika kujipatia mitaji , soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato .

1.0.1 Meneja wa Urasimishaji Rasilimali Mijini – (Nafasi -1)
Lengo na Jukumu Kuu :
Kujenga uwezo wa urasimishaji wa ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Ambazo zinatekeleza urasimishaji wa ardhi Tanzania . Aidha , anawajibika kusimamia na kuratibu shughuli za urasimishaji wa ardhi ambazo zinatekelezwa
nzania Bara .

1.0.2 Majukumu ya Msingi ni pamoja na:-i . Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za urasimishaji ardhi Mijini Tanzania Bara;
ii . Kuandaa na kufanya Mapitio ya Miongozo ya mafunzo kwa ajili ya kujenga uwezo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara;
iii . Kuandaa na Kuendesha mafunzo ya Urasimishaji wa ardhi Mijini kwa
Wataalam wa sekta ya ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za
Tanzania Bara;
iv . Kuandaa na kutekeleza Mpango Kazi na Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa urasimishaji wa ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara;
v . Kupokea na kuchambua taarifa za utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa ardhi Mjini ambazo zinatekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Tanzania Bara;
vi . Kubainisha na kutoa ushauri wa utatuzi wa changamoto ambazo
zinabainika wakati wa utekelezaji wa urasimishaji wa ardhi Mjini Tanzania Bara;
vii . Kufanya tathimini na kupendekeza maboresho ya Kisheria , Kanuni na
Kitaasisi ambazo zinabainika kuendelea kuwa kikwazo kwa Wananchi
katika kurasimisha ardhi zao Mijini na Majiji ya Tanzania Bara;
viii . Kuandaa na kutunza Kazi Data ya Rasilimali ardhi zilizorasimishwa katika Miji na Majiji ya Tanzania Bara;
ix . Kushirikiana na Mtaalamu wa Mawasiliano kwa Umma katika kuhamisisha na kujenga hamasa kwa wamiliki wa ardhi mijini ili waweze kurasimisha rasilimali zao;
x . Kuandaa na kufanya mapitio vigezo inavyotumika kuchagua ya kufanya
urasimishaji kila mwaka katika Miji na Majiji ya Tanzania Bara; na
xi . Kazi zingine ambazo utapangiwa na Msimamizi wako wa kazi .

1.0.3 Sifa na uzoefui . Awe na Shahada ya Upimaji na Ramani au Usimamizi na Utawala wa Masuala ya Ardhi ambayo inatambulika na Mamlaka ya Usimamizi wa Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania;
ii . Awe na uzoefu wa miaka mitano (5) kuhusu Sheria , Kanuni na Taratibu za Upimaji , Usimamizi na Usajili wa Ardhi za Tanzania Bara; na
iii . Awe na uzoefu katika utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa Ardhi Mijini na Majiji ya Tanzania Bara .

1.0.4 Aina ya Ajira :MKURABITA inatoa ajira ya Mkataba ambao unaweza kurejewa kutegemea na utendaji wa kazi utakaoneshwa wakati wa utekelezaji wa Mkataba wa awali .

1.0.5 Kituo cha KaziKituo cha kazi kwa sasa ni Dodoma lakini utekelezaji wa urasimishaji unafanyika katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa za Tanzania Bara .

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE .i . Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa wale tu ambao wapo ndani ya utumishi wa Umma .
ii . Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa .
iii . Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo , wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo;
iv . Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika;
v . Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma , maelezo , nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika .
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates .
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective
boards)
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni .
vi . Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo
za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA .vii . Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa
na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
viii . Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi .
ix . Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC . 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010 .
x . Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria .
xi . Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 30 Mei , 2019 .
xii . Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http ://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa
kufungua sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

MUHIMU : KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA
KAZIILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU KWA LUGHA YA
KISWAHILI AU KIINGEREZA .
ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA :

KATIBU ,
OFISI YA RAIS ,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
JENGO LA UTUMISHI ,
8 BARABARA YA KIVUKONI ,
S.L.P . 63100 ,
11404 DAR ES SALAAM-TANZANIA

IMETOLEWA NA
KATIBU ,
SEKRETATARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMA

Jobs

Leave a Reply